Historia ya uumbaji wa mbingu na dunia pamoja na uwepo wa mwanadamu hapa ulimwenguni, umeleta changamoto kubwa katika dini mbali mbali. Pia wanasayansi wanazo hoja zao zihusio uumbaji, uwepo wa Mungu, hukumu ya mwisho na Jehanamu. Dini zimekuwa nyingi kila kona ya mji au kijiji bali matokeo yake ni vurugu katika jamii. Kila dini inajisifu kuwa katika kweli huku chuki na malumbano ya kishuhudiwa kila leo. Lengo halisi ya Chaneli hii ni kuhamsha watu weusi kipekee na ulimwengu mzima kwa jumla katika kumtambua na kumtumikia Mungu aliye wa kweli. Dini zote zilizo katika dunia hii niza uhongo. Historia ya Biblia imebadrishwa na wazungu waliotafsiri maandiko matakatifu. Biblia kuanza kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo ni historia ya watu weusi ambayo wazungu walibadirisha. Nchi ya Israëli inapatikana Afrika ya kati, Kristo alikuwa mweusi, mitume wote walikuwa weusi, manabii wote walikuwa weusi, Adamu na Eva walikuwa weusi, Abrahamu, Isaka na Yakobo wote walikuwa weusi. Muda wa uamsho umefika.